Sambaza

S2Kizzy: Diamond, Wizkid Wana Kolabo Zaidi ya Mbili

PRODYUZA anayefanya vizuri kwenye tasnia kwa muda huu, S2kizzy, ameweka bayana kuwa nyota wa Nigeria, Wizkid na nguli wa Tanzania Diamond, wana nyimbo za pamoja kadhaa.

Kwenye mahojiano, prodyuza huyo alisema kuwa wasanii hao wawili wamekuwa wakifanya nyimbo mbalimbali katika miezi hii ya karibuni.

Mbali na hiyo pia amesema nyimbo hizo zimefanyika sehemu tofauti  ikiwemo Tanzania na Dubai.

Pia S2kizzy alisema kuwa nyimbo hizo zipo tayari japo hajaweka bayana lini zitatoka.

“moja ya kazi Zao ilianzia Dar es salaam na baadaye tukaenda kuimalizia Zanzibar, ilikuwa burudani kufanya kazi na nyota hao sababu wanaendana kwenye ufanyaji wao kazi,” alisema prodyuza huyo.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Diamond kufanya kazi na wasanii wa Nigeria kwa sababu ameshawahi kufanya kazi na Davido, Patoranking, Psquare na Tiwa Savage ne wengine.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey