Sambaza

Yemi Alade Aishauri Serikali Juu ya Corona

 

MSANII wa Nigeria mwenye tuzo mbalimbali, Yemi Alade, ametia neno kuhusiana na mwenendo wa Corona nchini humo.

Kwa kutumia mitandao yake ya kijamii, msanii huyo aliweka video ikionyesha umati wa watu jijini Lagos na kuandika kuwa ni vyema kama serikali itafanikisha kusogeza huduma ya upimaji kwa wingi.

Pia hakusita kuendelea kuiomba serikali iongeze ufanisi wa upatikanaji wa vifaa kinga kama sabuni, barakoa ambavyo vitatumika kwenye maeneo yote ya hadhara.

Mambo yameanza kurudi kama zamani kwenye nchi ya Nigeria baada ya serikali kulegeza sheria za kukataza watu kutoka nje.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey