Sambaza

RIHANNA AWEKA REKODI NYINGINE YA UTAJIRI UINGEREZA

Mwanamuziki kutoka Barbados anayeishi Uingereza kwa sasa, Robyn Rihanna Fenty (32) maarufu Rihanna kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya Wanamuziki tajiri wanaoishi Uingereza na kushika nafasi ya 3. Amehamia London mwaka 2019.

Rihanna ambaye pia ndiye Mwanamke wa kwanza kwa utajiri kwenye orodha hiyo ana utajiri wa takriban Tsh. Trilioni 1.325 (Paundi Milioni 468). Katika orodha hiyo amewapita wanamuziki kama Sir Elton John na Mick Jagger.

Utajiri wake umekua kutokana na kufanikiwa kwa biashara yake ya vipodozi vya Fenty Beauty na kuingia ubia katika biashara nyingine kama ‘Lingerie line’ inayohusika na nguo za ndani na uuzwaji wa albamu zake 8 za muziki.

Katika orodha hiyo, nafasi ya kwanza inashikiliwa na Sir Paul McCartney pamoja na Andrew Lloyd Webber ambao wote wana utajiri wa Paundi Milioni 800. Nafasi ya nne yupo Sir Elton John (£360m) na nafasi ya tano yupo Mick Jagger (£285m).

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey