Team Kiba Watoa Misaada Kwa Wahitaji
Tumezoea kuona wasanii wakisaidia watu wenye uhitaji kwa sehemu wanayoweza kwa kadiri walivyobarikiwa lakini imekuwa tofauti kwa wafuasi wa msanii Alikiba maarufu kama Team Kiba.
Wafuasi hao (Team Kiba) waliandaa hafla ndogo ya kusaidia wenye uhitaji ambayo waliipa jina la Team Kiba Corona Charity, ambapo walijichanga na kununua mahitaji kisha kuyakabidhi kwa wasiojiweza.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, @officialalikiba alionyesha wazi namna anavyojivunia kuwa na mashabiki wenye moyo wa kutoa na kusaidia wenye uhitaji na aliandika haya, “Nimefurahishwa sana na MUNGU atawalipa kwa mlichotoa, sio kila mtu ana moyo wa kutoa, najivunia sana kuwa na wafuasi wenye moyo na mapenzi kwa MUNGU hakika mmenipendeza na zawadi yenu niambieni nitoe lini?”