Sambaza

Nyimbo Zilizowapeleka Diamond, Alikiba na Harmonize Kimataifa

Alikiba na Diamond wamekuwa wakitawala muziki wa Bongo Fleva kwa miaka takribani saba tangu bifu lao lianze kushika vichwa vya habari.

Kila mmoja amekuwa na kipindi cha kung’aa zaidi kuliko mwingine kwa nyakati tofauti tofauti huku kila mmoja akiwa na mafanikio makubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Hata hivyo mwanzoni mwa ugomvi baina yao, wasanii hao walikuwa ni maarufu sana Afrika Mashariki na sio Afrika nzima kwa ujumla. Walikuwa ni wasanii wa kufanya kolabo za ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki tu mpaka pale walipofanikiwa kuachia nyimbo fulani zilizowapeleka kimataifa zaidi na kufikia kuwa maarufu Afrika nzima.

ALIKIBA

Msanii huyo alipumzika kufanya muziki kwa kipindi cha miaka takribani minne huku shabiki zake wakipiga kelele wakiomba ujio wake kwani bado walikuwa na kiu naye. Hatimaye mwanzoni mwa mwaka 2014 msanii Alikiba alirudi rasmi kukifuta vumbi kiti chake cha ufalme kama anavyodai na kuachia nyimbo mbili ambazo ni Kimasomaso na Mwana Dar es salaam. Mwana Dar es salaam ilifanya vizuri zaidi na kupelekea miezi kadhaa mbele kufanyiwa video na “Godfather” wa Afrika Kusini na kumtambulisha rasmi Alikiba kwenye soko la muziki wa kimataifa. Baada ya hapo zilifuata nyimbo nyingine  kali zilizopigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la muziki wa kimataifa kama Chekecha Cheketua, Aje, Lupela, Sudece me na nyinginezo.

DIAMOND PLATNUMZ

Mwaka 2009 aliingia rasmi kwenye tasnia ya muziki Bongo tena kwa kishindo kwelikweli na kibao chake cha Kamwambie ambacho kilitikisa Tanzania nzima. Ilimchukua miaka 4 tu kupenyeza muziki wa Bongo Fleva kwenye ramani ya kimataifa baada ya mwaka 2013 kuachia kibao cha “Number One” ambacho kilifanya vizuri sana kwa Afrika Mashariki mpaka pale alipoamua kufanya remix na msanii Davido kutoka Nigeria na kufanya vizuri sana Afrika nzima. Huo ukawa mwanzo wa safari ya kusisimua ya Diamond Platnumz ambapo aliendelea kutoa nyimbo ambazo zilibamba Afrika nzima na mashabiki wa Tanzania kuona kama wamepata mkombozi wa muziki wa Bongo. Nyimbo ambazo zilifatia ni kama Bum Bum, Nana, Kidogo na nyingine kibao ambazo zilisimika nguzo ya kimataifa.

HARMONIZE

Historia yake imeanza baada ya kumwaga wino kwenye kitabu cha wasanii wa Wasafi chini ya msanii Diamond Platnumz ambaye kwa kipindi hicho tayari alikuwa ameliteka soko la ndani na nje ya Tanzania na kuamua kumshika Harmonize mkono ili wasafiri pamoja kwenye njia ya mafanikio. Wimbo wa Aiyola ulimtambulisha vyema Harmonize kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania na hiyo ilkuwa mwaka 2015 mwishoni. Miezi kadhaa mbele yaani 2016 mwanzoni Harmonize alianza kupenya kwenye soko la kimataifa baada ya kutoa wimbo aliomshirikisha aliyekuwa bosi wake kwa kipindi hicho Diamond Platnumz. Hapo kila kitu kikabadilika kuanzia wapenzi hadi mavazi na hasa matamasha ya nje ya nchi yaliongezeka sana na kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii waliotoboa kimataifa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey