Magix Enga – ‘Nitampa Diamond Lamborghini Akijiunga na Lebo Yangu’
Prodyuza kutoka Kenya ameshika vichwa vya habari baada ya kusema kuwa anataka kumpa mkataba Diamond Platnumz na timu nzima ya Wasafi ili wawe chini ya lebo yake ya “Magix Empire.”
“Nina Lamborghini mahali fulani na kama Diamond atakubali kujiunga na Magix Empire nitampatia gari langu hilo bure,” alisema Prodyuza huyo.
Akielezea sababu za kutaka kumsajili Diamond na wasanii wake alisema kuwa aliposikiliza wimbo mpya wa kundi hilo kutoka Bongo aliona kuwa hawajautendea haki wimbo huo hasa akilinganisha na kazi zilizopita hivyo anataka kuwasaidia kwa kuwasajili ili wasipotee.
Toa Maoni Yako Hapa