Sambaza

Nasty C Aiwashia Moto Chombo cha Habari Ghana

Nyota wa Afrika Kusini amekasirishwa na chombo kimoja cha habari cha nchini Ghana kwa kile alichoelezea kuwa ni kugombanisha wachezaji wa timu moja.

Chombo hicho cha habari kilitoa mawazo yao juu ya utumbuizaji uliofanywa na Nasty C na Stonebwoy ambao wote walitumbuiza kwenye tamasha la “MTV Base Africa and Youtube Africa Day benefit concert.”

Kwa kutumia ukurasa wao wa twitter, chombo hicho cha habari kilisema “Diamond na Nasty C wamefanya vizuri lakini Stonebwoy amefanya vizuri zaidi.”

Nasty C hakutaka kuwalazia damu na alijibu “kwanini mnagombanisha wachezaji wanaochezea timu moja? Timu ambayo siku yake ndiyo hiyo (Yaani siku ya Afrika) hatuwezi kusherehekea watu wetu kwa amani?” aliandika Nasty C.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey