Sambaza

Bunge la Uganda Laingilia Kati Kufungiwa Kwa Eddy Kenzo Ivory Coast

Huenda msanii wa Uganda Eddy Kenzo akarejea nyumbani baada ya kujikuta ameshindwa kutoka nchini Ivory Coast baada ya “lockdown” ya nchi hiyo kumkumba akiwa humo hivyo kushindwa kutsafiri kurudi Uganda.

Spika wa bunge la Uganda mheshimiwa Rebbeca Kadaga alimuagiza waziri wa mambo ya nje kushughulikia suala la msanii huyo.

“Ningependa kuiomba wizara ya mambo ya nje kumsaidia kurudi nyumbani. Tumajipanga kumsaidia na pia kulipia gharama za yeye kurejea nyumbani,” alisema spika huyo huku akiahidi kuzungumza na Rais Yoweri Museveni kuwasaidia juu ya hilo.

“Yupo kwenye wakati mgumu sababu yupo kwenye nchi inayozungumza kifaransa, angalau angekuwa kwenye nchi inayozungumza kingereza mambo yangekuwa mepesi kwake,” aliongeza spika wa bunge la Uganda.

Msanii huyo alikwenda nchini Ivory Coast kufanya tamasha tarehe 16 Machi 2020 ambapo ugonjwa wa Corona ulipolipuka Afrika nchi hiyo ilifunga mipaka yake hivyo kushindwa kurudi Uganda.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey