Sambaza

Kim Kardashian Asikitishwa na Kifo Cha George Floyd

“Kama wengi wenu nimekasirika, tena ni zaidi ya kukasirika nimechukizwa sana,” haya ni baadhi ya maneno aliyoyaandika mke wa Kanye West, Kim Kardashian akielezea hisia zake juu ya kifo cha mmarekani mweusi aliyeuwawa na polisi kwa kuwekewa goti kwenye shingo yake kwa takribani dakika 8.

Nyota huyo wa mitindo na mjasiriamali alizungumza hisia zake kwa kutumia ukurasa wake wa instagram na kueleza ni namna gani hali imezidi kuwa mbaya kwa jamii ya watu weusi nchini humo.

“Kwa miaka mingi, kwa kila mauaji ya watu weusi wasio na hatia nimekuwa nikijaribu kutafuta lugha nzuri ya kutoa pole zangu za dhati kwa waliofiwa,” alianza Kim “ila kwa yanayoendelea yamenifanya nitambue kuwa hii sio vita ninayoweza kupambana mwenyewe.”

“Nimechoshwa kuona wakina mama, baba, kaka, dada na watoto wanapata wakati mgumu sababu wapendwa wao wameuwawa bila hatia kisa ni weusi,” aliongeza Kim Kardashian West.

“Japokuwa sijui maumivu yao ila naweza kutumia sauti yangu kupaza sauti za wale waliokuwa wakinyanyasika kwa muda mrefu,” alimalizia Kim huku akiweka na njia za kufata ili kuweza kuchangia.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey