Rick Ross Kupima Covid-19 Kila Akitaka Kuonana na Watoto Wake
Rapa William Leonard maarufu kama Rick Ross amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya mama watoto wake kuiomba mahakama kumpa katazo la kuonana na watoto wake mpaka apime virusi vya Corona.
Mwanamama huyo ameiambia mahakama kuwa rapa huyo hajawa akizingatia suala la kujitenga na kukaa ndani ili kuepuka kunaswa na virusi hivyo huku akiionyesha mahakama picha na video za msanii huyo akiwa anasafiri mara kwa mara ndani ya nchi.
Akizungumzia suala la malezi anasema kuwa japo Rick Ross hajaonana na watoto wake kwa muda wa miezi sita lakini msanii huyo amekuwa akiihudumia familia hiyo vyema na kusisitiza anachohofia ni usalama wa watoto hao.
Toa Maoni Yako Hapa