Sambaza

Kanye West, Kim Kardashian Watishia Kufungua Kesi Dhidi ya Aliyekuwa Mlinzi Wao

Rapa Kanye West na mkewe Kim Kardashian wamemuambia aliyekuwa mlinzi wao kuwa watafungua kesi kumshtaki endapo hatoacha kuzungumzia mambo yao ya kifamilia.

Wiki kadhaa zilizopita mlinzi huyo ambaye alifukuzwa na familia hiyo kuacha kufanya nao kazi, alikwenda kwenye mahojiano na kudai kuwa Kanye West alikuwa na sheria kali na alikuwa ni mtu wa kukasirikia vitu vidogo.

Hata hivyo familia ya Kanye West imesema kuwa madai ya mlinzi huyo ni ya uongo na pia amevunja makubaliano ya kimkataba baina yao ambayo yanamnyima haki mlinzi huyo kuzungumzia jambo lolote linalohusiana na familia ya Kanye na Kim.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey