Sambaza

Masaka Kids Wazidi Kung’aa, You Tube Yaipa Tuzo

Kundi la kucheza muziki kutoka Uganda “Masaka Kids” wameendela kung’aa ndani ya mwaka huu ambapo wamefikisha subscribers milioni moja kwenye jukwaa la kuuza muziki la You Tube.

Kundi hilo ambalo limezidi kujipatia umaarufu duniani kote kwa kucheza muziki na pia kushirikishwa kwenye video za miziki mbalimbali limepata barua maalumu kutoka You Tube ikiwapongeza kwa hatua hiyo.

Mafanikio haya yamekuja wiki kadhaa tu tangu walipopewa shavu na msanii nguli duniani Drake ambaye aliweka kundi hilo kwenye kurasa zake za kijamii na kulisifu kwa namna walivyocheza wimbo wake wa ‘Toosie Slide.’

“Tunajua kuwa kwa mnavyogusa maisha ya watu ni heshima na tuzo tosha. Ila tunafurahishwa na mnayoyafanya na ni matarajio yetu mtaipokea tuzo hii ya heshima tunayowapa,” ilisomeka sehemu ya barua iliyoandikwa na You Tube.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey