Sambaza

Kifo Cha George Floyd Chafanya YG Kuimba Wimbo Unaowatukana Polisi

Rapa kutoka Compton Marekani YG alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kuimba wimbo uliokuwa ukipinga utawala wa Donald Trump huku jina la wimbo huo ukiwa ni tusi lililoelekezwa moja kwa moja kwa Rais huyo wa Marekani.

Baada ya kuwa na maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi ambapo maanadamano hayo yamesababishwa na kifo cha George Floyd aliyeuwawa na polisi, msanii YG ameamua kuingia studio na kurekodi wimbo unaowatusi polisi ambao tayari umekamilika na ametangaza kuuachia siku za karibuni.

Japo bado haijawa bayana ni lini haswa wimbo huo utatoka, lakini inatarajiwa mwisho wa wiki hii utatoka huku akiwa sio msanii pekee aliyeimba kuhusiana na yanayoendelea Marekani kwa sasa.

Wasanii wengine walioimba nyimbo kuhusu kifo cha George Floyd ni Conway the Machine, Ty Dolla Sign na wengine.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey