Sambaza

SZA Aelezea Namna Alivyobaguliwa ‘Nililengwa na Machozi’

Wakati maandamano ya kupinga  ubaguzi wa rangi yakiendelea nchini Marekani, msanii wa miondoko ya RnB SZA amesimulia mkasa uliomkuta siku za karibuni na kuonyesha umma kuwa watu weusi hawaheshimiki nchini humo.

Kupitia ukurasa wake wa twitter msanii huyo alianza kwa kuandika “Jambo la ajabu mno limetokea leo,” alisema SZA. “Jamaa mmoja ametaka kunitoa nje ya (super market) akihisi mimi ni miongoni mwa waandamaji wanaofanaya vurugu,” aliendelea msanii huyo.

Shabiki mmoja alimuuliza SZA kama jamaa huyo ni mzungu na SZA alijinu kuwa ndiyo alikuwa ni mzungu huku akiongeza na kusema “katika kipindi kama hiki ninataolewa nje nikidhaniwa kuwa nataka kuleta vurugu, nililengwa na machozi.”

“Sikutaka kuwakatalia polisi kwa sababu ningeonekana kama mfanya vurugu kweli, sitaki kuishi hivyo tena nataka kulia na kupiga mayowe kama nikijisikia kufanya hivyo,” alimalizia mrembo huyo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey