Sambaza

Fat Joe: Jay Z Hakumtoa Drake Kwenye ‘All The Way Up’

 

Rapa nguli Fat Joe amekanusha vikali taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Jay Z ndiye aliyefanya Drake asitokee kwenye remix ya wimbo wa all the way up.

Fat Joe alisema kwenye moja ya mahojiano kuwa “wimbo ule ilipaswa Drake pia awepo kwa sababu alikuwa akiniomba beat aifanyie kazi lakini Jay Z alisema kutokana na historia yetu itapendeza kama wimbo itakuwa wa watu watatu tu yaani Fat Joe, Jay Z na Remy.”

Vyombo vingi vya habari vilinukuu kauli hiyo na kusema kuwa Jay Z alikwamisha mchongo wa Drake kushiriki kwenye kolabo hiyo ambayo ilifanya vizuri.

Fat Joe alitumia ukurasa wake wa twitter na kusema kuwa taarifa ya kuwa Jay Z ndiye aliyefanya Drake asitokee kwenye wimbo huo sio kweli sababu Jay Z hakufahamu mtu yeyote aliyekuwa anatakiwa kufanya kazi ile bali alitaka tu uwe wimbo wetu pekee.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey