Sambaza

Nchi Tatu Zinazofuatilia Zaidi Muziki wa Diamond

Akiwa kama msanii aliyetazamwa zaidi kuliko msanii yeyote Afrika Mashariki ndani ya mwaka mmoja tangu Mei 1, 2019 hadi Mei 1, 2020 mtandao wa You Tube umebainisha ni nchi gani zilizompa Diamond watazamaji wengi.
Muwakilishi wa You Tube akiwa anaongea na kampuni ya chati za muziki “Billboard” alisema kuwa watazamaji wengi wa Diamond Platnumz wanatokea Kenya.
Tanzania imechangia asilimia 20 kati ya watazamaji wote wa Diamond Platnumz kwa mwaka mmoja huku ikiwa ndiyo Nchi ya pili na Marekani ikishika nafasi ya tatu.
Mbali na video za nyimbo zake, msanii huyo amekuwa akiweka pia matukio mbalimbali kama matamasha yake, purukushani za utengenezaji wa video zake na mambo mengine pia.
Mpaka sasa Diamond ameweka takribani video 600 kwenye mtandao huo wa You Tube.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey