Sambaza

Snoop Dog Akiri Kuwa Hajawahi Kupiga Kura Maishani Mwake

Mwaka 2020 umekuwa mwaka wa matukio mengi lakini pia ni mwaka wa uchaguzi kwenye nchi mbalimbali ikiwemo Marekani.

Katika hali ya kushangaza, rapa Snoop Dog amesema kuwa mwaka huu ndio utakuwa mwaka wake wa kwanza kupiga kura sababu hajawahi kupiga kura siku za nyuma.

“Sijawahi kupiga kura maishani mwangu lakini mwaka huu nadhani lazima nipige kura sababu nimeshindwa kuvumilia kumuona huyu rais (Trump) madarakani,” alisema rapa huyo.

“Kwa muda mrefu walinidanganya kuwa siwezi kupiga kura sababu nina historia ya jinai lakini kumbe hiyo ilipita na ninaruhusiwa kupiga kura,” aliongeza uncle Snoop.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey