Sambaza

Mteja Ataka Neno ‘Black Lives Matter’ Lisionekane Kwenye Mtandao wa Amazon, Jeff Bezos Ajibu

Jeff Bezos hajali ni kiasi gani anaweza kupata hasara au ni wateja wanagapi atawakosa kwa kukemea vitendo vya kibaguzi.

Tajiri huyo namba moja duniani ametumia ukurasa wake wa instagram kumjibu mteja wake aliyemtumia barua pepe akisema kuwa hapendezwi kuona neon “Black Lives Matter” kwenye mtandao wa Amazon.

Mteja huyo aliyefahamika kwa jina moja la “Macy” aliandika barua pepe hiyo na kusema kuwa “All Lives Matter” akiwa anamaanisha kuwa maisha ya kila mmoja ni muhimu na kusisitiza kuwa tajiri huyo anafanya biashara na watu wengi mbalimbali hivyo sio vizuri kuweka neon linaloonyesha kujali watu weusi tu.

Jeff alijibu kwa kusema “Nitapingana na wewe kwenye hili, natambua maisha ya kila mmoja ni muhimu lakini Black Lives Matter ni sauti ya kupinga ubaguzi wa rangi. Nina motto wa miaka 20 na sina hofu kuwa ipo siku atakabwa hadi kufa lakini wazazi weusi wana hofu hiyo na nataka ujuwe kuwa ninakubaliana na maandamano haya naa sitabadili uamuzi huo.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey