Sambaza

Kenya Wafanya Upelelezi Kupotea Kwa Vifaa Vya Kuzuia Corona

Mamlaka za Kenya zinafanya upelelezi juu ya kupotea kwa vifaa tiba vya kuzuia mambukizi ya Covid-19 ambapo vifaa hivyo vililetwa kama msaada kutoka kwa serikali ya China.

Vifaa hivyo kutoka China vilijumuisha barakoa, vipima joto, mavazi maalumu ya kujikinga ambavyo vina gharama ya dola za Marekani milioni 2.

Kenya imepokea mamilioni ya pesa na vifaa tiba kutoka kwa mataifa na mashirika mbalimbali kwa ajili ya kupambana na gonjwa la Covid-19.

Misaada hiyo ni pamoja na ule wa Jack Ma kutoka China, IMF na nchi mbalimbali za ulaya.

Hata hivyo serikali imekumbana na maswali mengi kutoka kwa wananchi wake juu ya namna gani misaada hiyo inatumika wakati wataalamu wa afya wanalalamika kukosekana kwa vifaa vya kujikinga na vya kupima ugonjwa huo.

Waziri wa afya nchini humo, Mutahi Kagwe amekiri kuwa kuna janja janja kwenye makao makuu ya wizara hiyo na kuapa kulifanyia kazi.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey