Sambaza

DARASA – Shigongo Akabidhi Simu Janja Kwa Mshindi

 

Jimson Mwakalindile amekabidhiwa zawadi ya simu kwa niaba ya mshindi wa shindano la “Jishindie Smartphone na Darasa” ndugu Richard Boniphace ambaye ni mkazi wa Tunduma.

Mkurugenzi wa kampuni ya Global Group ndugu Eric Shigongo ambaye pia ni mwalimu wa kipindi cha DARASA akishirikiana vyema na mwalimu Rodrick Nabe wamekabidhi simu hiyo aina ya TECNO POP2 yenye thamani ya shilingi laki moja na elfu sitini (160,000).

“Naomba nisiongee mengi nikala muda wa DARASA lakini ninashukuru sana kwa zawadi hii,” alisema Richard Boniphace ambaye alizungumza hayo kwa njia ya simu huku akiwa anatazama mubashara muwakilishi wake akikabidhiwa simu hiyo kupitia Global TV Online.

“Napenda nimpongeze mshindi toka Tunduma na nashukurua sana kwa kuendelea kufuatilia kipindi hiki, na niombe tu muendelee kualika watu wengine waje kusikiliza darasa hili ili tujifunze kwa pamoja,” Eric Shigongo alizungumza baada ya kumkabidhi mshindi zawadi ya simu.

Hii ilikuwa ni zawadi iliyotokana na droo ya kwanza iliyochezeshwa Juni 16, 2020 na kumpata mshindi huyo ambaye alitangazwa siku hiyo.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey