Sambaza

Sholo Mwamba – ‘Man Fongo Afanye Biashara Nyingine Sio Muziki’

Nyota wa Singeli Sholo Mwamba amesema kuwa Man Fongo kwa sasa aache tu mziki na kufanya biashara nyingine kwani mziki umemshinda.

Akizungumza na vipaza sauti vya 255 Global Radio aliyasema hayo baada ya kuulizwa kuwa ni msanii gani angemtoa kwenye muziki wa singeli maana ni kama hamna anachofanya.

Sholo Mwamba alijibu kuwa “Man Fongo atuachie muziki wetu afanye mambo mengine Yule sio msanii Yule ni DJ.”

Pia aliongezea kuwa Man Fongo itabidi awe dj wa “Jully sauti ya Kinanda” ambaye ni msanii anaepewa sapoti na Sholo Mwamba.

Aidha Sholo Mwamba amefunguka kuhusu matamanio yake ya kumiliki wasanii na kuwa bosi wao ila amesema changamoto anayokutana nayo ni kuwa kwa sasa hana uelewa wa kutosha juu ya masuala hayo ila akipata uelewa wa kutosha basi atafanya hayo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey