Sambaza

Malawi Kupiga Kura Leo ‘Kwa Mara Ya Pili’

Baada ya matokeo ya awali kukataliwa na upinzani kwa kile walichosema kulikuwa na wizi wa kura, hatimae leo wanachi wa Malawi watapiga kura ya kumpata Rais.

Kinyang’anyiro hicho kilileta sitafahamu kwa miezi kadhaa baada ya matokeo ya uchaguzi wa Mei 2019 kupigwa chini ambapo kwenye uchaguzi huo Rais Peter Mutharika ndiye aliyeibuka mshindi kabla ya wapinzani kwenda mahakamani na kupinga matokeo hayo.

Mchungaji Lazarus Chakwera ndiye anayegombea Urais kwa tiketi ya upinzani huku mgombea wa tatu ni Peter Kuwani ambaye anaonekana kutokuwa na ushawishi mkubwa katika kinyang’anyiro hicho.

Sheria mpya ndiyo itakayotumika ambapo sasa mshindi atapaswa kuwa na 51% ya kura. Nchi hiyo ipo katika wakati mgumu uku umasikini na ukosefu wa ajira ukiwa ni wa hali ya juu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey