Sambaza

Mrisho Gambo Ampongeza RC Iddy Kimanta

Aliyekuwa mkuu wa mkoa ndugu Mrisho Gambo ametumia ukurasa wake wa twitter kumpongeza mkuu mpya wa mkoa huo Mzee Iddy Kimanta ambaye aliteuliwa na Rais Magufuli na kula kiapo cha utiifu jana tarehe 22 Juni 2020.

Mrisho Gambo ndiye aliyegawa kijiti cha wadhifa huo baada ya kuenguliwa na Rais John Magufuli tarehe 19 Juni 2020 na ameonyesha kuwa ameridhika na maamuzi ya Rais baada ya kumpongeza RC mpya wa jiji la Arusha.

Mrisho Gambo aliandika ““Hongera sana Mzee wangu Iddy Kimanta Kwa kuteuliwa na kuapishwa Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, nakutakia kila la heri na Mungu akakusimamie kwenye kazi zako, Rais Magufuli kafanya mambo mengi na makubwa Arusha.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey