Sambaza

Rashford Aingia Mkataba na Jay Z

Kampuni kubwa ya muziki Roc Nation ambayo ipo chini ya Jay Z imejikita kwenye michezo kwa miaka ya hivi karibuni na imekuwa ikipiga hatua kubwa kubwa kila kukicha.

Kampuni hiyo imetangaza kuingia mkataba na mchezaji wa Manchester United Marcus Rashford ambaye kwa siku za karibuni ameshika vichwa vya habari baada ya kupaza sauti yake kuhusu watoto kutokupata chakula.

“Tunatafuta wale vijana ambao wanasimama kwa vitu zaidi ya michezo tu, huyu ni kijana wa miaka 22 aliyesimama na kusema hakuna motto aanayepaswa kulala bila kupata chakula, hata ukiwa mtu mchoyo zaidi duniani huwezi kupingana na hili” alisema meneja wa Roc Nation Sport.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey