Sambaza

Grace Matata Kuzaliwa Tena Kwenye Album Yake Mpya

Msanii mwenye sauti nyororo na mashairi adimu kwenye tasnia ya muziki Tanzania Grace Matata, amefunguka kuwa anakwenda kuzaliwa upya kwenye album yake inayotarajiwa kutoka mwezi wa 7 ambayo itaitwa “Rebirth.”

Grace ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Bongo 255 cha +255 Global Radio ambapo aliweka wazi kuwa album hiyo ipo njiani huku akiwasisitiza mashabiki zake kuendelea kuburudika na “Me and You” ambao ndio wimbo wake mpya.

Hata hivyo Grace Matata hakusita kuzungumzia mahusiano yake na marapa wa Tanzania baada ya kuulizwa kama alikatazwa na label yake ya zamani kufanya kazi na marapa tofauti na walio ndani ya lebo hiyo.

“Ilikuwa rahisi kufanya kazi na wasanii wa kurap nikiwa M-Lab lakini baada ya hapo sikuwa na mahusiano ya karibu na marapa wengine na haikuwa katazo kutoka labo ya M-Lab,” alijibu Grace Matata.

Aidha kuhusiana na sakata la kubaniwa Grace alijibu na kusema “mimi sijawahi kusema nabaniwa kwa sababu mwisho wa siku wale waliopo hapo juu sio kwamba wamepewa hiyo nafasi wamefanaya juhudi kuwa pale, kwahiyo ukitaka niwepo pale inamaana unataka nimtoe mmoja niwepo mimi jambo ambalo sio sawa.”

Pia Grace Matata alianika mapenzi yake kwa msanii wa WCB Mboso na kusema kuwa yeye ni shabiki mkubwa sana wa Mboso na kusema anaheshimu sana maandishi ya mboso.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey