Sambaza

Patrick wa Kanumba Afunguka Mahusiano Yake na Jeniffer

Othman Njaid maarufu kama Patrick Kanumba amefunguka kuhusu tetesi za kuwa mpenzi wa Jenifer na mengine mengi.

Katika mahojiano aliyofanya na kipindi cha Katambuga kinachoruka hewani kila siku za jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa nne hadi sita kamili mchana kupitia +255 Global Radio Patrick alisema kuwa yeye na Jenifer hawana uhusiano wowote wa kimapenzi na asingependa kuwepo na huo uhusiano kwani utaaribu ukaribu wao.

Patrick Akiwa Na Watangazaji Wa Katambuga (@+255 Globa Radio)

“Mimi na Hanifa (Jennifer Kanumba) hatujawahi kuwa wapenzi. Tumekuwa marafiki kwa muda mrefu hivyo kama tukiingia kwenye mapenzi tunaweza tukaja kugombana ikafanya hata familia kugombana pia kitu ambacho nisingependa kitokee,”  alisema Patrick Kanumba.

Hata hivyo iliwabidi watangazaji kubadili mada kwani Patrick alinekana kama hajatoa majibu ya ukweli hivyo wakamuuliza kuhusu ugumu anaoupata kufanya kazi na watu wengine tofauti na Kanumba aliyezoea kufanya naye kazi.

Patrick alijibu “Hamna ugumu sana kufanya kazi na watu wengine tofauti na Kanumba lakini pengo lake lipo kwa sababu hakuwa tu mtu tunayefanya naye kazi lakini pia alikuwa mlezi.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey