Sambaza

Kisa Kanye West Mashabiki Wamuita Snoop Dog ‘Mnafki’

Snoop Dog huenda akaamua kuzima mtandao wa simu yake ili asione yanayoendelea huko.

Hii ni baada ya mashabiki kumshambulia na kumuita mnafki baada ya rapa huyo kuweka video ikimuonyesha rapa Kanye West akiwa na prodyuza Dr Dre wanaandaa wimbo pamoja.

Kwenye video hiyo Snoop Dog alisikika akisema “Kanye West ana bonge la wimbo, shhhh Kanye na Dr Dre wametengeneza wimbo mzuri mno na unakuja hivi karibuni.”

Sifa alizommwagia Kanye West ndizo zilizoleta ukakasi kwa mashabiki kwani miaka kadhaa iliyopita Snoop Dog alimponda sana Kanye West kwa kitendo cha kumuunga mkono Rais Donald Trump, hivyo mashabiki wanaona kama Snoop Dog ameungana na Kanye West.

“Uncle Snoop ni mnafki, anafanya tofauti na maneno yake, nilidhani anamchukia Kanye West,” ilisomeka jumbe moja ya shabiki mtandaoni.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey