Sambaza

Wizkid, Burna Boy Wang’aa BET

Usiku wa kuamkia leo umekuwa mzuri kwa wasanii kutoka Nigeria Burna Boy na Wizkid baada ya kunyakua tuzo za BET.

Burna Boy ameshinda tuzo hiyo ya “Best international act” ambapo alikuwa kwenye mchuano mkali na Inoss B na Sho Madjozi ambaye amekuwa akimtupia Burna Boy lawama kuwa amemfanyia fitina ili asishinde tuzo hiyo.

Kwa upande wa Wizkid tuzo aliyoipata ni kupitia mgongo wa Beyonce ambapo wimbo alioshirikishwa na mwanadada huyo uitwao “Brown Skin Girl” ndio uliochukua tuzo ya HER.

Mwanadada kutoka Zimbabwe Sha Sha amewashangaza wengi baada ya kuibuka mshindi wa tuzo ya chaguo la watazamaji na kumgaraza Rema ambaye wengi waliamini ndiye atakayeshinda tuzo hiyo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey