Sambaza

Jacqueline Mengi Aanika Umri Wake, Mipango ya Ndoa

Mwanadada Jacqueline Mengi amejibu maswali ya shabiki zake kupitia mtandao wa Instagram ambapo aliwapa fursa ya kuuliza chochote na wengi wakatiriria.

Vitu ambavyo huenda vikawashangaza wengi ni namna alivyoweka wazi umri wake kitu ambacho wadada wengi hupenda kutosema miaka yao.

Shabiki yake mmoja aliuliza umri wake na Jacqueline akamjibu “nina miaka 41 ila najihisi kama nina miaka 21.”

Pia mrembo huyo ambaye ni mama wa watoto wawili mapacha hakusita kuongelea masuala ya ndoa ambapo shabiki mmoja alimuuliza, “Utaolewa tena?” nay eye akajibu “Sijui, ngoja tuone Mungu amenipangia nini.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey