Kifo cha Mwanamuziki Chazua Maandamano Ethiopia
Msanii Hachalu Hundesa ambaye amekuwa akitumia muziki kufikisha ujumbe wa kisiasa kwenye jamii ameuwawa kwa kupigwa risasi kwenye makao makuu ya Ethiopia, Addis Ababa.
Maandamano yamezuka nchini Ethiopia baada ya polisi kuthibitisha kifo cha msanii huyo kilichotokea jumatatu. Kuanzia jumanne asubuhi wananchi wenye hasira kali wameandamana kwenye maandamano yaliyosababisha vifo takribani 50.
Hachalu aliwahi kufungwa kwa sababu ya kuipinga serikali mwaka 2018 ambapo maandamano hayo yalifanikiwa kuiondoa serikali iliyokuwa madarakani.
Waziri mkuu wa Ethiopia amesema “Nawapa pole wote ambao tuko nao pamoja katikaa maumivu ya kuondokewa na nyota iliyokuwa iking’aa Hachalu Hundesa.”
Toa Maoni Yako Hapa