Lockdown Ikiisha Tu, Rick Ross Anatua Uganda
Miezi miwili iliyopita lebo ya “Swangz Avenue” ilidhibitisha kuwa msanii wa rap Kutoka Marekani Rick Ross anatarajiwa kuingia Uganda na kufanya tamasha kubwa.
Hii ilitiwa nguvu na Rick Ross mwenyewe baada kuweka video mtandaoni inayomuonyesha akidhibitisha taarifa hiyo.
Baada ya hali ya “lockdown” kuendelea Uganda kwa muda mrefu sasa, imebidi watu kuanza kuuliza juu ya uwezekano wa tamasha hilo kufanyika au ndio limeairishwa.
Promota wa tamasha hilo aliwatoa mashabiki hofu na kusema “Rick Ross anatamani sana kuja Afrika tena. Anatamani kuja kwenye ardhi ya mama yake na kufanya tamasha kubwa na kuwashukuru wote wanaopambana na ugonjwa wa Corona, hivyo hili janga likipita tu atakuja.”
Kwa mujibu wa mkuu wa biashara wa tamasha hilo, litaitwa “Uganda Benefit Concert” huku likiwa ni maalumu kwa wafanyakazi wa afya na kuwashukuru kwa kazi kubwa wanayofanya.