Meneja wa Alikiba Ajibu Tuhuma Za Kufukuzwa
Esi Lovey ambaye ni meneja wa Alikiba ameelezea tetesi zinazosema kuwa Alikiba ameuondoa uongozi wote akiwemo Esi.
Mapema kulikuwa na hizo tetesi ya kuwa Alikiba hakufurahishwa na utendaji kazi wa uongozi wake huo hivyo kuamua kukatisha mkataba nao.
Hata hivyo kwenye mahojiano aliyofanya, Esi Lovey amesema kuwa kama kuna mabadiliko yoyote basi Alikiba atayaongelea na kusisitiza kuwa vyombo vya habari vinapaswa kuangalia zaidi muziki wa Alikiba na sio uongongozi.
“Ali ni msani, na focus inatakiwa iende kwa msani… Ali kama CEO anajua kila kitu. Akiwa na kitu kipya cha kuzungumuza atazungumza. Ukiona hajakizungumza its not yet the time for the audience to know the information,” alisema meneja huyo.
Toa Maoni Yako Hapa