Ndugu Wafukua Maiti Iliyozikwa Miezi 3 Iliyopita
Ndugu wa marehemu Tulizo Konga mkoani Mbeya, imewabidi kufukua maiti ya ndugu yao aliyefariki Machi 25 na kuzikwa Machi 28 baada ya kuwa na mashaka juu ya kifo cha ndugu yao huyo.
Ndugu hao walipata kibali cha kufanya hivyo kutoka kwa mamlaka za kisheria.
Sababu zilizowapelekea ndugu hao kufukua maiti ni kuwa wametilia mashaka namna kifo cha ndugu yao kilivyotokea ndiyo maana waliamua kufuatilia hatua zote lengo likiwa ni kuujua ukweli kama ndugu yao alifariki kifo cha kawaida ama aliuawa, kutokana na mazingira ya kifo hicho kuwa ni ya mashaka.
Toa Maoni Yako Hapa