Sambaza

Vladmir Putin Kuwa Rais Mpaka 2036

Rais wa Urusi Vladmir Putin ameshinda kura ya maoni ambayo itamuwezesha kukaa madarakani hadi 2036.

Mpaka sasa 90% ya kura zilizopigwa zimekwisha hesabiwa huku 78% ya kura hizo kwa mujibu wa tume ya uchaguzi zikikubali Rais Putin kuendelea kubaki madarakani.

Rais huyo mpaka sasa amekaa madarakani kwa miaka 20 sasa na amekuwa akihudumu kama Rais na Waziri mkuu kwa wakati mmoja na kumfanya kuwa kiongozi alikaa madarakani kwa muda mrefu zaidi nchini Urusi.

Kura ya maoni hiyo imepigwa ili kuidhinisha katiba itakayomuwezesha Putin kugombea tena katika uchaguzi kwa mara awamu mbili zaidi na kuweza kubakia madaraakani hadi 2036, muhula wake wa hivi sasa unamalizika miaka 4 ijayo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey