Meek Mill Ashtakiwa Kuiba Nyimbo Mbili
Msanii Meek Mill anatuhumiwa kuiba nyimbo mbili za msanii mwingine na kuzitumia kama zake.
Lebo ya Dream Rich Entertainment imefungua mashtaka dhidi ya Meek Mill na lebo ya msanii huyo Atlantic Records kwa kukiuka sheria za haki miliki na kutumia nyimbo hizo kwenye album yake iitwayo “Championship” iliyotoka mwaka 2018.
Dream Rich wamesema kuwa Meek Mill amekuwa akidharau wito wa kutaka kuonana ili wazungumze juu ya nyimbo hizo hivyo wamefungua kesi wakidai dola elfu 75 kwa kila kosa hivyo kufanya kudai kwa jumla dola laki 3 ambazo ni takribani milioni 700 za Tanzania.
Toa Maoni Yako Hapa