Sambaza

Kanye West: Sikubaliani na Trump Tena

Moja kati ya habari kubwa mwaka huu ni msanii Kanye West kutangaza nia ya kugombea Urais wa Marekani.

Forbes wamefanya mahojiano maalumu na msanii huyo na kufunguka mambo mengi ikiwemo kuvua kofia nyekundu ambayo ni ya chama cha Republican cha Donald Trump.

“Simuungi tena mkono Trump,” alisema Kanye West na alipoulizwa ni chama gani atagombea kati ya Republican na Democrat alijibu na kusema hatokuwa sehemu ya chama chochote kati ya hivyo.

“Ningegombea kama mwanachama wa Republican kama Trump asingekuwepo pale, ila sitagombea kwa chama hiko sababu trump yupo pale,” alisema msanii huyo.

Kuhusu kwanini mpaka sasa hajafanya taratibu zozote alijibu na kusema anazungumza na wataalamu wa hayo mambo.

“Sipendezwi na kauli ya Joe Bidden kuwa kama hutompigia kura basi wewe sio mtu mweusi, naona ni utawala mwingine wa wazungu kutuambia nini tuafanye” aliongeza Kanye West.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey