Sambaza

Anusurika Kuuawa na Ndugu Kisa Ndizi

Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni na hii imethibitika baada ya kijana mmoja aitwaye Issa huko kisiwani pemba kukatwa katwa na panga na ndugu yake wa damu na kuamua kujifanya amekufa ili ndugu huyo amuache.

Issa anasema kuwa alikuwa shambani kwake na binti mdogo wa kaka yake na ghafla wakasikia mtu anakata migomba akaamua kwenda kuangalia na akastaajabu kukuta ni mtu anayemfahamu na kumuuliza “kwanini uibe badala ya kuomba?”

Mwizi Yule alimuuliza “kwani unasemaje?” Issa akamjibu huku anachukua ndizi zile “nataka ndizi zangu?” ndipo hapo mwizi Yule ambaye ni ndugu yake alipomshambulia kwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Issa anasema ilimbidi ajifanye amekufa ili jamaa yake huyo amuache na bahati nzuri binti Yule wa kaka yake alikimbia kwenda kuita watu na hivyo Issa aliwaishwa hospitali na kupatiwa huduma huku aakiachiwa ukilema wa milele.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey