Sambaza

Kanye West Ni Mgonjwa Wa Akili? Kim Kardashian Afunguka

Mke wa msanii Kanye West amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na ugonjwa wa akili wa mume wake, ambapo tetesi zimekuwa zikisema Kanye West anaugua ugonjwa ambao unaadhiri akili.

Kim Kardashian amesema kuwa hajawahi kuzungumzia masuala hayo sababu anailinda familia yake, na anaheshimu haki za Kanye West ila imebidi aongee sababu kumekuwa na gumzo kubwa.

“Ni mtu mwenye akili nyingi lakini ni ngumu kumuelewa hasa ukizingatia ni msanii na ni mtu mweusi ambaye amempoteza mama na amekuwa akitengwa kwasababu ya ugonjwa wake huu,” alisema Kim.

“Walio karibu na Kanye West wanafahamu moyo wake na wanajua kuwa muda mwingine maneno yake hayaendani na dhumuni lake,” aliongeza Kim Kardashian.

Mwisho Kim Kardashian aliomba jamii na vyombo vya habari viwape nafasi na huruma katika kipindi hiki kigumu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey