Sambaza

Mr Blue: “Diamond Sio Mshkaji Wangu, Alikiba Nilianza Naye Zamani”

Rapa wa Bongo Mr Blue amefunguka mbele ya kamera za global tv online na kusema kuwa Diamond Platnumz sio mshkaji wake kiasi cha mashabiki kuwaona pamoja kila mahali.

“Diamond ni mtoto wa Dar es salaam na mimi pia ni wa hapa, tumekutana kwenye mitikasi ya kutafuta pesa. Kuna jamaa mmoja anaitwa Papaa misifa ndiye aliyenikutanisha na Diamond na kuniambia kuwa tumsaidie nikaweka mchango wangu niliojaliwa baadae akaendelea na maisha yake, sio mshakji wangu ‘banka to banka’ (Bega kwa Bega),” alisema Mr Blue.

Mr Blue aliendelea kusema kuwa hana mshkaji wa karibu kwenye tasnia ya muziki bongo ambaye ni mshkaji bega kwa bega kabisa bali washkaji zake ni watoto wake.

Mbali na hayo Mr Blue pia amesema itafika wakati ataachana na muziki na hiyo ndio sababu ya kutoa nyimbo nyingi ndani ya muda mfupi.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey