Sambaza

Tanzania Imefikaje Uchumi Wa Kati

Julai 1 2020 Benki kuu ya dunia iliitangaza Tanzania kuingia kwenye uchumi wa kati.

Julai 2 2020 msemaji wa serikali Dkt. Hassan Abasi amezungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma na kusema takwimu za kipato cha waliopata ajira ndio sehemu kubwa iliyochukuliwa na Benki ya dunia kuthibitisha kwamba pato la Watanzania limeongezeka.

Katika mkutano wake na waandishi, Dkt Abasi amesema ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji wa megawati 2500 kama mojawapo ya mambo yaliyosababisha kuimarika kwa uchumi wa taifa hilo na kusema kuwa mradi huo umeleta ajira 3500.

”Katika miaka 59 tunayoelekea ya Uhuru na katika miaka mitano ya uongozi wa rais Magufuli kama kuna eneo tumewekeza kwa kiasi kikubwa na limesaidia sana kuchemsha uchumi ni katika ujenzi ambao wengine wanaita maendeleo ya vitu. Kwa mfano unapozungumzia mradi wa umeme wa Rufiji umebuni ajira ya zaidi ya 3500”, alisema afisa huyo wa serikali.

Uanzishwaji wa viwanda umekuwa chachu ya kufikia kwenye uchumi wa kati na msemaji huyo wa serikali amesema “hivi sasa kwa mfano tuna uwezo wa kuunganisha matinga humu nchini, kuunganisha mabasi kuzalisha nondo ,mabati na kadhalika”

Ripoti ya Benki kuu nchini Tanzania mapema mwaka 2017 ilifichua kwamba serikali iliokoa takriban $430m (£330m) kwa kupunguza safari za ughaibuni kati ya mwezi Novemba 2015 hadi Novemba 2016.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey