Aliyedhaniwa Kuwa Ndiye Mwenye Umri mkubwa Zaidi Afariki
Mwanaume mmoja (Fredie Blom) nchini Afrika Kusini aliyedhaniwa kuwa ndiye mwenye umri mkubwa zaidi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 116.
Nyaraka za utambulisho wake zinaonyesha kuwa alizaliwa mwaka 1904 ingawa hilo halikuwahi kuthibitishwa na rekodi za Gunnes za dunia.
Miaka ya 1918, Fredie, alinusurika vita ya kwanza ya dunia na vita ya mapambano ya dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Katika mahojiano aliyofanya mwaka 2018 na BBC, Blom, alisema hakuna siri maalumu ya kuishi maisha marefu kwani hata yeye alikuwa mvuta sigara.
Familia ya Bwana Blom amesema alikufa kifo cha kawaida mjini Cape Town Jumamosi.
Toa Maoni Yako Hapa