Harmonize Aahidi Makubwa Siku Ya Mwananchi
Msanii wa Bongo Fleva, Harmonize, amewatoa hofu mashabiki wake pamoja na mashabiki wa Yanga kuelekea maadhimisho ya siku ya mwananchi yanayotarajiwa kufanyika Agosti 29, 2020 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.
“Watu wanauliza kwamba Harmonize ataingia vipi pale Taifa, mimi sipendi kusema maneno mengi sana, lakini hii itakuwa best performance ever,” alisema Harmonize
Tamasha hili litakuwa hitimisho la wiki ya wananchi iliyoandaliwa na timu ya soka ya Yanga huku ikiwa na dhumuni la kuwakutanisha mashabiki pamoja na timu na kutambulisha wachezaji watakaohudumu msimu mpya wa 2020/2021.
Toa Maoni Yako Hapa