Sambaza

Ommy Dimpoz, Christian Bella, Wachinjaji Wapya Bongo Star Search

Baada ya kuwepo kwa sintofaham kama tamasha kubwa la kutafuta vipaji Tanzania ‘Bongo Star Search’ litakuwepomwaka huu, sasa ni rasmi kuwa tamasha hilo lipo na wachinjaji (majaji) wapya ni Ommy Dimpoz na Christian Bella.

Akizungumza na wana habari, Madam Rita, ambaye ndiye muasisi wa shindano hilo amewatambulisha wasanii hao wawili kuwa watakuwa miongoni mwa majaji kwenye msimu huu wa 11.

“Kila jaji atakuwa na timu yake ambapo timu hizo zitashindana vikali sana,” alisema Madam Rita. Jaji wa muda mrefu na nguli wa muziki Tanzania, Master Jay, amesema kuwa katika shindano hilo la timu za majaji yeye ndiye atashinda kwani wakina Ommy Dimpoz na Bella ni watoto tu labda wamshinde kupendeza.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey