Sambaza

Femi One: “Mimi Ni Shabiki Wa Harmonize”

MSANII kutoka Kenya, Femi One, ambaye amevuma sana kwa wimbo wake wa ‘Utawezana’ amefika jijini Dar esa salaam ambapo alikuwa na show yake jana Agosti 30.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Femi alifunguka kuuzimia muziki wa Harmonize na kuweka wazi kuwa anatamani kufanya naye kazi.

“Napenda sana muziki wa Harmonize, nimeongea na uongozi wangu ila sina uhakika kama wamezungumza naye,” alisema Femi One.

Pia aligusia suala la Vanessa Mdee kuacha muziki na kusema, “niliposikia ‘Podcast’ ya Vanessa niliumia sana kwani hata Kenya bado kuna tatizo hilo la wasanii wa kike kuchukuliwa kwa mtazamo tofauti.”

Rapa huyo alisindikizwa na bosi wake ambaye ni Msanii pia kutokea Kenya ‘King Kaka.’

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey