Sambaza

Kwa Mamilioni Haya, Mondi Katoboa

NASIBU Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz, amekuwa ni nembo ambayo inatangaza vizuri muziki wetu kwa hapa Afrika.

Katika burudani, unaweza kusema kwa sasa amekuwa ni mwanamuziki ambaye ameliteka sana soko la Bongo Fleva. Wengi waliomtambua na ngoma kama Kamwambie, Mbagala, Lala Salama, Kizaizai, Binadamu na nyingine kibao ambazo zilifanya poa sana na kumtambulisha vizuri.

Diamond ambaye ni bosi wa Lebo kubwa ya muziki hapa Bongo ya Wasafi Classic Baby (WCB), ameendelea kuiteka ramani ya muziki wa Bongo Fleva kwa kali za Mondi ambazo zimefanya poa kwa kujikusanyia mamilioni ya watazamaji kwenye mtandao wa YouTube.

YOPE REMIX

Yope Remix imetoka miezi kumi na moja iliyopita, lakini imefanya poa sana kwa kutazamwa na watazamaji milioni 109 mpaka sasa na kuvunja rekodi kwa ukanda wa hapa Afrika Mashariki.

INAMA

Inama ni ngoma ambayo imetoka mwaka mmoja uliopita na kufanya poa kwenye mtandao wa YouTube kwa kutazamwa na watazamaji milioni 68.

AFRICAN BEAUTY

African Beauty tangu imetoka, ni miaka miwili sasa na tayari imejikusanyia kijiji cha watazamaji milioni 51 mpaka sasa na kuendelea kushikilia rekodi ya ngoma kali ambayo bado haijachuja.

MARRY YOU

Marry You ni ngoma ambayo iliachiwa miaka mitatu iliyopita na kufanya poa kwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 44.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey