Sambaza

Rihanna Kuhusu Chriss Brown, “Tunapendana”

Rihanna amefunguka rasmi juu ya urafiki wake na aliyekuwa mpenzi wake Chriss Brown.

Wawili hao wamewahi kuwa kwenye mahusiano ambapo hayakuisha vizuri baada ya Chriss Brown Kumpiga Rihanna na kumuachia makovu kadhaa mwilini mwake.

Akizungumza kwenye podcast ya Oprah, Rihanna amefunguka kuwa yeye na Chriss wamendelea kuwa na maelewano mazuri tangu walipoachana.

“Tumekuwa tukiufanyia kazi urafiki wetu,” alisema Rihanna “kwa sasa sisi ni marafiki wakubwa, tumejenga imani baina yetu na tunapendana sana na huenda tutapendana milele,” aliongeza Rihanna.

“Kiukweli ninampenda, alikuwa mpenzi wa maisha yangu na nafahamu alinipenda pia ila ninafurahi ana amani maana sitakuwa na amani kama hana amani,” alimaliza Rihanna.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey