Sambaza

Lil Wayne, Drake Kufanya ‘Tour’ ya Kibabe Pamoja

Drake na Lil Wayne kila mmoja ni nguli wa muziki na wamefanya makubwa kwenye maisha yao ya muziki lakini wakiungana huwa wanakuwa na nguvu isiyozuilika, si unakumbuka Young Money?

Basi wawili huenda wakafanya tena shoo ya pamoja na kuizunguka dunia pamoja.

Akifanya mahojiano na mtangazaji B Dot, Meneja wa Lil Wayne alisema kuwa wawili hao wamelizungumzia suala hilo na huenda likafanyika tena.

“Wamezungumza kuhusu hilo, nadhani tunatakiwa kufanya hivyo tena,” alisema meneja wa Lil Wayne.

Lil Wayne na Drake walifanya matamasha ya pamoja mwaka 2014 ambapo tamasha hilo lilikuwa likiitwa ‘Drake vs Lil Wayne Tour’ ambapo lililenga kutangaza ujio wa album zao (Nothing Was The Same Ya Drake na The Carter IV ya Lil Wayne).

Hata hivyo hata kama tamasha hilo litakuwepo basi halitakuwa siku za karibuni kwani bado vizuizi vya Covid 19 vitakwamisha kwa sasa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey