Tiwa Savage Aeleza Siku Aliyotamani Kuacha Muziki
Ugumu humkuta yeyote. Hii inathibitishwa na Tiwa Savage baada ya kusimulia jinsi alivyokata tamaa na kutaka kuacha muziki.
Kwenye mahojiano aliyofanya na New York Times, nyota huyo wa Nigeria alisema kuwa mwaka 2010 alikuwa karibu kuacha muziki baada ya kutoa wimbo wake wa “love me, love me.”
Wimbo huo ulifungiwa na shirika la habari Nigeria kitu kilichopelekea hata baadhi ya matamasha yake kuahirishwa na kufanya msanii huyo akate tamaa kabisa na masuala ya muziki.
Akielezea sababu iliyomsukuma kurudi kwenye biashara ya muziki alisema, “baada ya kufanya maamuzi ya kuacha, kulikuwa na wasichana wengi waliokuwa wakinitumia ujumbe mara nimependa hereni zako, au mara nimependa tattoo yako na hapo ndipo niliposema acha nirudi kwa ajili ya wasichana hawa.”
“Mpaka sasa ninawahamasisha wasichana wengi lakini wao ndio walionihamasisha kurudi kwenye muziki,” alisema Tiwa Savage.