Sambaza

Kanye West Atoa ya Moyoni, “Lebo za Universal, Sony ni Utumwa”

Hakuna asiyefahamu kuwa akili za Kanye West anazijua yeye mwenyewe. Namna zinavyofanya kazi ni Mungu pekee ajuaye.

Kanye amekuwa kwenye mahusiano yasiyo mazuri baina yake na watu wengi amabao wengine walikuwa marafiki zake wa karibu.

Ni Kanye huyu huyu alimnyang’anya ‘mic’ Taylor Swift mbele ya umati na kumuambia kuwa hakustahili kupokea tuzo aliyopewa badala yake alistahili kupewa Beyonce.

Ni Kanye huyu huyu aliwahi kusema kuwa Rais mstaafu George Bush hakuwa akijali kuhusu watu weusi tena aliyaongea maneno hayo akiwa mubashara kwenye runinga.

Sasa kwa wakati huu, Kanye West ameonekana kama kuna mambo mengi yanayoendelea kwenye kichwa chake na kuamua kutumia ukurasa wa Twitter na kueleza yaliyojaa kifuani mwake.

Ameandika, “Nataka kuona mikataba ya kila mtu kwenye lebo za Universal na Sony,” kisaha akendelea kusema “Sitakaa pembeni na kuangalia watu wangu wakifanywa watumwa. Tasnia ya muziki na NBA ni utumwa wa zama hizi” kasha akamalizia kusema “mimi ni Musa wa muda huu.”

Lebo za muziki za Universal na Sony zimekuwa zikitupiwa lawama japo sio kwa ukubwa lakini kumekuwa na malalamiko ya chini chini kuwa wananyonya wasanii. Lebo hizo zimewahi kufanya kazi na miamba nguli ya Afrika kama Alikiba, Diamond, Davido na wengine wengi.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey