Sambaza

Ibrah Ashukuru Harmonize Kwa Zawadi ya Gari -(Picha +Video)

Msanii anayetumikia Lebo ya Konde Gang iliyo chini ya mwanamuziki Harmonize, Ibraah, leo ametinga ndani ya +255 Global Radio na kufunguka mambo mbalimbali ikiwemo ishu ya kupewa gari na bosi wake huyo.

Kupitia Kipindi cha Bongo 255 kinachodili na muziki na burudani zote ndani na Bongo, Ibraah amemshukuru Harmonize kuanzia kumtoa hadi juzikati alipompa zawadi ya gari.

“Mimi ni wa kwanza kumiliki gari nyumbani kwetu kwa hiyo ni jambo kubwa sana, siwezi kuacha kumshukuru Harmonize.

“Ibraah ni mtoto kutoka kwenye familia masikini, nimesoma elimu ya msingi kisha nikaingia mtaani nikaanza kuuza CD hadi nikachoka.

“Baada ya kuchoka kuuza CD nilianza kuuza makoti ya mitumba hadi siku moja Uncle wangu Duke aliponiambia Harmonize anapatikana maeneo ya Kijuweni (Sinza).

“Nimehaso sana na nilitamani sana kutoboa na nimsaidie mama yangu huku mjomba wake akiniambia nisikate tamaa.

Alipoulizwa kuhusu kufunikwa na msanii Zuchu wa WCB ambaye walitambulishwa wakati mmoja, Abraah amesema; “Hakuna ubaya, sote ni wasanii wa Tanzania. Huwezi kumbishia shabiki vile anavyooona.”

Kuhusu uwezekano wa yeye kufanya kolabo na Diamond, Ibraah amesema;

“Kolabo ikiwepo tunafanya kwa sababu ni msanii mkubwa na lengo ni kuufikisha muziki wetu watu.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey